
Katika ujumbe alioutoa Jumatatu, Brigedia Jenerali Esmail Qa’ani aliandika: “Mapambano ya kishujaa ya muqawama wa Hizbullah nchini Lebanon yamethibitisha kuwa simulizi zinazotolewa na utawala wa Kizayuni unaoua watoto, zikidai mwisho wa muqawama na kuangamizwa kwa Hizbullah, si chochote ila ni uongo mtupu.”
Ameongeza kuwa: “Nyuga zote za muqawama zimesimama bega kwa bega na Hizbullah ya kishujaa kwa nguvu na mshikamano mkubwa zaidi kuliko wakati wowote.”
Kauli hizo zimekuja katika muktadha wa ukiukaji unaoendelea wa usitishaji mapigano wa siku kumi uliotangazwa mapema mwezi huu, huku ukiwa unakabiliwa na majibu thabiti kutoka upande wa Hizbullah.
Wakati huohuo, Tel Aviv imekuwa ikijaribu kuishinikiza Lebanon kuelekea kuivua silaha Hizbullah, sambamba na kueneza propaganda zinazodai kudhoofika kwa uwezo wa kijeshi na azma ya harakati hiyo, madai ambayo yamekanushwa waziwazi na Hizbullah.
Jenerali Qa’ani amebainisha kuwa kampeni dhidi ya Hizbullah imehusisha “matumizi makubwa ya rasilimali fedha pamoja na kuhamasishwa kwa nguvu kazi na zana za kijeshi kwa kiwango kikubwa.” Aidha, amebaini kuwa utawala huo umekuwa “ukipoteza fedha za walipa kodi wa Marekani” katika juhudi zake za kuidhoofisha Hizbullah, akirejelea msaada wa kifedha unaotolewa na Marekani kwa Tel Aviv katika hatua zake za uchokozi dhidi ya Lebanon.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa “utawala wa Kizayuni leo uko katika hali ya udhaifu na kukata tamaa zaidi kuliko wakati wowote mbele ya uimara na ubunifu wa vijana jasiri wa Lebanon.”
Kamanda huyo aliongeza kuwa katika miaka ya karibuni, utawala huo umeshindwa kumaliza kwa mafanikio vita vyote ulivyoanzisha, akiutaja kuwa “mshindwa mkubwa” na “aliyedhalilika” katika matukio hayo ya uchokozi.
4348908