Akizungumza na IQNA, Gholamreza Karimu Mkuu wa Tume ya Kitaifa ya ISESCO nchini Iran amesema shughuli hizo zinajumuisha kuwafunza waalimu wa Qur'ani, kuinia kiwango cha taasisi za Qur'ani katika nchi mbali mbali hasa barani Afrika sambamba na kustawisah ufundishaji lugha ya Kiarabu ambayo ni lugha ya Qur'ani.
ISESCO ni taasisi ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC na ilianzishwa Mei mwaka 1979. ISESCO ndio taasisi kubwa zaidi ya Kiislamu katika uga wa kimataifa inayoshughulikia masuala ya elimu, sayansi na utamaduni.