IQNA

ISESCO yasisitiza kuhusu nafasi ya Mashhad katika ustawi wa utamaduni

10:48 - January 26, 2017
Habari ID: 3470813
IQNA:Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni (ISESCO) amesizitiza nafasi ya mji mtakatifu wa Mashhad katika ustawi wa utamaduni wa mwanadamu.
ISESCO yasisitiza kuhusu nafasi ya Mashhad katika ustawi wa utamaduni

Akizungmza Jumanne wakati wa kuzinduliwa Mashhad kama mji mkuu wa utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu barani Asia mwaka 2017, Bi. Amina al-Hajri amesema mjio huwa wa kaskazini mashariki mwa Iran kwa muda mrefu umekuwa kitovu cha sayansi, fasihi, elimu, sanaa na utamaduni.

Amesema hadhi ya mji wa Mashhad kama eneo la ziara ni yenye umuhimu mkubwa kwani ni sehemu ya pili duniani ambayo hutembelewa na mamilioni ya Waislamu wafanya ziara kila mwaka.

Al-Hijra amesema ni fakhari kubwa kwake kuhudhuria sherehe hiyo na kuelezea matumaini yake kuwa Mashhad utapata mafanikio zaidi kama mji mkuu wa utamaduni wa Kiislamu na kuwa nembo ya ustaarabu na ubunifu. Amesema ISESCO inatumia vigezo vigumu sana kuchagua mji kama mji mkuu wa utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu na kwamba Mashhad iliweza kutimiza vigezo vyote.

Katika mkutano wa saba wa ISESCO, ambayo ni taasisi cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, uliofanyika Algiers mwka 2007, mji mtakatifu wa Mashhad ulichaguliwa kuwa mji mkuu wa utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2017. Mji wa Mashhad hupokea wafanya ziara milioni 27 Wairani na milioni mbili wa kigeni ambao hufanya zaira katika Haram ya mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Ridha AS kila mwaka.

3566143

captcha