IQNA

'Kuwait, mji mkuu wa kiutamaduni Ulimwengu wa Kiislamu 2016'

14:43 - January 19, 2016
Habari ID: 3470066
Kumezinduliwa shughuli za 'Kuwait, mji mkuu wa kiutamaduni Ulimwengu wa Kiislamu 2016' katika hafla iliyofanyika Jumatatu hii katika mji wa Al Salmiya nchini Kuwait.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hafla hiyo ilihudhuriwa na Jabir Al Mubarak Ahmad Al Sabah.

Akizungumza katika kikao hicho, Salman Sabah Salim Al Hamud Al Sabah, waziri wa habari wa Kuwait na Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Utamaduni, Sanaa nchini humo amesema: "Kuchaguliwa Kuwait kama mji mkuu wa kiutamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2016 ni jambo linaloashiria umuhimu wa nchi hiyo katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha amepongeza jitihada za Abdulaziz Othman Al-Twaijr Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kiislamu la Utamaduni, Elimu na Sayansi ISESCO katika uga wa kuimarisha mshikamano wa nchi wananchama katika utekelezwaji harakati za Kiislamu.

Amesema Kuwait itatumia fursa iliyojitokeza kueneza na kuhimiza thamani za Kiislamu za maelewano, kusameheana, mahaba, amani sambamba na kuariofisha Uislamu wa wastani.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Sheikh Ahmad Tayyib, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar.

3468662

captcha