IQNA

Msikiti wateketezwa moto mjini Chicago, Marekani

9:05 - November 29, 2019
Habari ID: 3472239
TEHRAN (IQNA)- Msikiti umeteketezwa moto mjini Chicago nchini Marekani katika tukio linaloaminika kutekelezwa na magadidi wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Moto uliibuka Jumatano Alasiri katika msikiti unaojulikana kama Masjid al Farooq katika mtaa wa 8950 S. Stony Island Ave. Calumet Heights. Eneo la ndani ya msikiti liliharibiwa vibaya na moto huo.

Maafisa wa polisi wanasema uchunguzi wa awali umebaini kuwa msikiti huo uliteketezwa moto na kijana aliyekuwa akitoka shuleni.

Uchunguzi ungali unaendelea lakini hakuna mtu yeyote aliyekamatwa hadi sasa.

Tukio hilo linaonekana kuwa ni muendelezo wa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu kote Marekani.

Kwa ujumla kote Marekani kumeshuhudiwa ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu na hilo linatokana na sera za kibaguzi za mtawala wa nchi hiyo, Donald Trump.

Wakati wa kampeni zake, Trump alikuwa ametaka Waislamu wazuiwe kikamilifu kuingia Marekani.

Baraza La Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) linasema tokea Donald Trump achaguliwe kuwa rais wa Marekani, Waislamu nchini humo wameshuhudia ongezeko kubwa la ubaguzi dhidi yao huku wakishambuliwa na kubugudhiwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

3469986

captcha