IQNA

Nchi za Kiarabu zataka Israel iwaachilie huru wafungwa Wapalestina

12:43 - March 25, 2020
Habari ID: 3472601
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na asasi zingine za dunia kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel uwaachilie huru Wapalestina inaowashikilia katika magereza yake ili wasiambukizwe ugonjwa wa COVID-19 au corona ambao umeenea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Said Abu Ali, amesema ni jambo la dharura kuwalinda wafungwa, hasa katika zama kama hizi za janga la ugonjwa wa COVID-19, ambao umeenea kwa maambukizi kote duniani.

Amesema jamii ya kimataifa inapapswa kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel uwaachilie huru wafungwa 5,000 Wapalestina wakiwemo wazee, watoto 180 na wanawake 43.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, nayo pia hivi karibuni iliziomba taasisi za kisheria za kimataifa zichukue hatua za kuwanusuru mateka wa Kipalestina katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na kukithiri maambukizo ya virusi vya corona katika jela hizo.

Msemaji wa harakati ya Hamas, Abdullatif al Qanou amesema kuwa kitendo cha taasisi inayosimamia jela za utawala wa Israel  cha kuzuia hatua za kudhibiti maambukizi ya corona na wakati huo huo kuzuia kuingizwa dawa za kujikinga na maambukizo katika jela hizo ni jinai dhidi ya binadamu. 

Wakati huo huo Harakati ya Wafungwa wa Palestina pia imesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unazuia wafungwa wa Kipalestina wasipewe vifaa vya dharura zikiwemo dawa na vifaa vya afya vya  kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona. 

Vilevile Kamati ya Masuala ya Wafungwa wa Kipalestina wiki iliyopita ilitangaza kuwa, utawala wa Kizayuni ulimtuma mgonjwa mmoja raia wa Palestina katika jela ya Asqalan kwa daktari wa Kiisraeili ambaye alikuwa ameathiriwa na virusi vya corona kwa ajili ya kupatiwa matibabu.  Baada ya kurejea jela mateka huyo wa Kipalestina aliamiliana na idadi kubwa ya wafungwa ndani ya jela hiyo na kuna uwezekano ameeneza maambukizo kwa watu wengine wengi.  

Hadi sasa zaidi ya watu 1,238 walioambukziwa corona katika utawala wa Kizayuni wa Israel na mmoja miongoni mwa amefariki.

3470982

captcha