iqna

IQNA

IQNA – Harakati ya Palestina ya Mapambano ya Kiislamu, Hamas, imelaani vikali uvamizi wa kichokozi uliofanywa na walowezi wa Kiyahudi katika eneo la msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, jijini Quds (Jerusalem) ikieleza kuwa ni sehemu ya juhudi za Israel za kufuta utambulisho wa Kiislamu wa eneo hilo takatifu.
Habari ID: 3480781    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/03

IQNA-Kiongozi mmoja wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amejibu matamshi ya kijuba ya rais wa Marekani, Donald Trump aliyetangaza nia ya Marekani ya kuuteka Ukanda wa Gaza na eti kuugeuza kuwa eneo huru, akimwambia, Ghaza si bidhaa ya kupigwa mnada.
Habari ID: 3480691    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/16

IQNA-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina , Hamas, imelinganisha vitendo vya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya kimbari ya Rwanda, huku ikisifu hatua ya Umoja wa Afrika Afrika kumfukuza balozi wa utawala wa Israel kutoka mkutano maalum wa kumbukumbu uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia.
Habari ID: 3480514    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/08

IQNA – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Palestina, Hamas, imetoa wito wa maandamano duniani kote wiki hii kwa ajili ya kuwasaidia na kufungamana na Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, mji mtakatifu wa al-Quds na Msikiti wa al-Aqsa. Katika Siku ya Kimataifa ya Quds.
Habari ID: 3480442    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/26

IQNA – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Palestina Hamas ililaani mauaji ya Salah al-Badrawil yaliyofanywa na utawala katili wa Israel, ikisisitiza kuwa kwa kila shahidi, mwenge wa Muqawama unazidi kuwa mkali.
Habari ID: 3480421    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/23

Matukio ya Palestina
IQNA-Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema upayukaji na vitisho vya Trump vinavuruga makubaliano ya kusitisha mapigano kwani vinauchochea utawala wa Kizayuni wa Israel kutotekeleza wajibu wake.
Habari ID: 3480318    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/06

IQNA – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imewataka Wapalestina kufika katika Msikiti wa Al-Aqsa katika al-Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiwahimiza kushiriki katika ibada, ikiwemo itikafu.
Habari ID: 3480283    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/01

IQNA-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa wito kwa Wapalestina, Waarabu, Waislamu na watu huru kote duniani kushiriki katika harakati ya kimataifa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, ili kupinga mipango ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuwaondoa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kulikalia kwa mabavu eneo hilo.
Habari ID: 3480219    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/14

IQNA-Harakati ya Mpambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imekariri upinzani wake dhidi ya matamshi yaliyotolewa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu suala la kuwahamusha makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza kwa kisingizio cha kulijenga upya eneo hilo.
Habari ID: 3480213    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/13

IQNA – Mkuu wa Ofisi ya Mashujaa, Waliojeruhiwa, na Mateka wa wanamapambano wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ameelezea kuachiliwa kwa mateka wa Palestina kuwa sherehe ya kitaifa na alama ya umoja.
Habari ID: 3480105    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/27

Jinai za Israel
IQNA – Jumla ya wanawake na watoto 90 wa Kipalestina waliachiliwa kutoka magereza ya kuogofya ya Israel mapema Jumatatu kama sehemu ya kubadilishana wafungwa iliyohusishwa na makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3480083    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/20

Muqawama
IQNA – Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa utawala wa Kizayuni umelazimika kusitisha mapigano na Harakati ya Kiislamu ya Ukombozi wa Palestina, Hamas, huko kwa sababu ya udhaifu na kukata tamaa. Hii ni moja ya heshima za mstari wa mbele wa upinzani, alisema Hujjatul-Islam Gholam Hossein Mohseni Ejei, akihutubia mkutano wa 13 wa "Gaza; Alama ya Muqawama" jijini Tehran.
Habari ID: 3480073    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/18

Kadhia ya Palestina
IQNA-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kuwa, kulazimika utawala wa Kizayuni kukubali kusimamisha vita na kukomesha mauaji yake ya kimbari dhidi ya wananchi wa Ghaza, ni matunda ya Muqawama (mapambano ya Kiislamu) na kusimama imara wananchi wa ukanda huo kwa zaidi ya miezi 15.
Habari ID: 3480062    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/16

Muqawama
IQNA- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) imeidhinisha pendekezo la kusimamisha mapigano kwa Ukanda wa Gaza ambayo yamefikiwa kwa upatanishi wa Misri na Qatar.
Habari ID: 3480060    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/15

Kadhia ya Palestina
IQNA-Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa wito wa kufanyika " hamas a kubwa ya umma" kwa lengo la kuondoa mzingiro wa kinyama uliowekwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3479949    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/24

Muqawama
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa Marekani na washirika wake wanakoseka kikamilifu wanapodhani kwamba Muqawama umeishiwa nguvu na umefika ukingoni.
Habari ID: 3479913    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/17

Muqawam
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa pongezi kwa mashahidi wa muqawama (mapambano ya Kiislamu) na kusema kwamba wameleta heshima katika kambi ya muqawama.
Habari ID: 3479715    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/07

Muqawama
IQNA - Mchambuzi wa kisiasa wa Lebanon ameuelezea shahidi Yahya Sinwar kama kamanda wa muqawama wa kupigiwa mfano ambaye alifanya juhudi bila kuchoka katika njia ya umoja wa Kiislamu wa Jihadi.
Habari ID: 3479621    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/20

Rambirambi
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kufuatia kuuawa shahidi kamanda shujaa wa Mujahidina, Yahya Sinwar, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, HAMAS, na kusisitiza kuwa: "Kama vile safu ya Muqawama (mapambano ya Kiislamu) haikuacha kusonga mbele kwa kuuawa shahidi shakhisia wake mashuhuri, vivyo hivyo haitakoma kwa kuuawa shahidi Sinwar."
Habari ID: 3479615    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/19

Muqawama
IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, Yahya Sinwar amemuandikia barua kiongozi wa harakati ya Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah, akiahidi kwamba harakati hiyo ya muqawama au mapambano ya Kiislamu "itasalia imara" katika njia ya kuushinda utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3479428    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/13