IQNA

Mahakama yaondoa marufuku ya Hijabu katika mji mmoja Sweden

22:30 - November 18, 2020
Habari ID: 3473371
TEHRAN (IQNA) – Mahakama nchini Sweden imeondoa marufuku ya vazi la Kiislamu la Hijabu katika shule za mji mmoja wa kaskazini mwa nchi hiyo ya bara Ulaya.

Kwa mujibu wa taarifa, Mahakama ya Rufaa ya Malmo imebatilisha uamuzi wa mahakama ya chini kuwa Hijabu inakiuka katiba na uhuru wa dini.

Marufuku hiyo ya Hijabu ilikuwa imewekwa katika mji wa Skurup, ambao uko katika jimbo la Skane kusini mwa nchi hiyo.

Manispaa ya Skurup ilikuwa imepiga marufuku Hijabu kwa wanafunzi walio chini ya umri wa miaka 13 mwaka jana.

Katika miaka ya hivi karibuni nchi nyingi za Ulaya zimekuwa zikitekeleza kampeni za kupiga marufuku vazi la Kiislamu la Hijabu. Waislamu wanajitahidi kutumia sheria za nchi hizo kukabiliana na wimbi hilo la chuki dhidi ya Uislamu.

3473165

Kishikizo: sweden hijabu waislamu
captcha