IQNA

WaislamuSweden wataka katiba izuie kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini

21:59 - September 14, 2020
Habari ID: 3473168
TEHRAN (IQNA) –Waislamu nchini Sweden wametaka katiba ya nchi hiyo ifanyiwe marekenisho iliiwe na kipengee cha kupiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.

Sheikh Hussein Farah Warsame, mmoja kati ya viongozi wa Waislamu nchini Sweden amesema wanataka iwe marufuku nchini Sweden kuvunjia heshima vitabu vitakatifu kama vile Qur'ani, Bibilia na Torati ya Mayahudi.

Ombi hilo limekuja siku chache baada ya mjumbe wa chama chenye misimamo mikali cha Hard Line nchini Denmark kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa kuchoma moto nakala ya kitabu hicho katika kitongoji cha wabaguzi wa rangi cha Rinkeby mjini Stockholm.

Askofu Mkuu wa Sweden na maafisa wengine wa ngazi za juu wa kanisa la nchi hiyo wametoa taarifa wakilaani kitendo cha kundi moja lenye misimamo mikali la nchi hiyo cha kuivunjia heshima Qur'ani tukufu.

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Baraza la Kikristo la Sweden ambalo limelaani vikali hatua ya chama cha mrengo wa kulia cha Hard Line ya kukivunjia heshima kitabu kitukufu cha Qur'ani. 

Katika taarifa hiyo wachungaji kumi wa ngazi za juu wa Kanisa la Protestanti la Sweden wakiongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Antje Jackelén wamelaani hujuma inayolenga matukufu na itikadi za Waislamu. 

Askofu Mkuu Antje Jackelén amesema viongozi wa kidini wa Sweden wananajitenga kikamilifu na kitendo hicho cha kuvunjia heshima kwa makudusi itikadi za wafuasi wa dini nyingine.

Taarifa ya viongozi hao wa Kanisa la Protestanti nchini Sweden imesema kuwa  kuvunjia heshima kitabu cha Qur'ani ni kitendo cha kihayawani. 

3472554

Kishikizo: sweden ، waislamu ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :