IQNA

Bango la kuarifisha Hijabu katika barabara za Marekani

15:11 - January 06, 2021
Habari ID: 3473529
TEHRAN (IQNA) – Waislamu katika mji mmoja nchini Marekani wanaendeleza kampeni ya kuelimisha umma kuhusu vazi la Kiislamu la Hijabu na faida zake.

Katika kampeni hiyo, bango kubwa lenye kufafanua kwa kifupi kuhusu Hijabu yamewekwa katika Barbara kubwa katika mji wa Dallas.

Bi. Ruman Sadiq, mwakilishi wa Kituo cha Kiislamu Amerika ya Kaskaizni katika mji wa Dallas jimboni Texas anasema wanaamini kuwa, njia bora zaidi ya kuelimisha umma kuhusu Hijabu na wanawake Waislamu ni kufanya mazungumzo kwa mbinu mbali mbali.

Anasema mabango hayo waliyoweka ni njia ya kuwasiliana na wasiokuwa Waislamu ili kuondoa taswira potovu waliyonayo kuhusu Hijabu na wanawake Waislamu.

Amesema mbali na kuweka mabanvo, pia wamezindua vibanda kote Texas ambavyo vitakuwa na wataalamu watakaojibu maswali ya umma kuhusu Uislamu na Waislamu.

Katika kampeni hiyo, wasiokuwa Waislamu wanahimizwa kuvaa Hijabu kwa siku nzima. Aidha wale wenye masuali kuhusu haki za wanawake Waislamu wanajibiwa. Bi. Sadiq anasema kampeni hiyo imefanikiwa sana kwani imebainika kuwa wengi hawakuwa na taarifa sahihi kuhusu Uislamu.

Kampeni hiyo ni mradi wa pamoja wa Kituo cha Kiislamu Amerika ya Kaskaizni katika mji wa Dallas na Taasisi ya GainPeace.

Hii si kampeni ya kwanza ya GainPeace ya kuelimisha watu kuhusu Uislamu. Mwezi Februari 2017 taasisi hiyo iliweka bango la kuelimisha umma kuhusu Sira ya Mtume Muhammad SAW.

3945856

Kishikizo: hijabu waislamu marekani
captcha