IQNA

Iran yataka Waislamu waungane katika kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

20:56 - March 18, 2021
Habari ID: 3473745
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ulimwengu wa Kiislamu una wajibu wa kupambana vilivyo misimamoo mikali ndani yake. Amesema, ni wajibu wa ulimwengu huo kuunganisha nguvu zake kupambana na watu wenye aidiolojia za chuki na za kuwakufurisha Waislamu wengine.

Dk Mohammad Javad Zarif amesema hayo katika kikao cha jana Jumatano cha ngazi za juu cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kilichofanyika kwa njia ya Intaneti mjini New York Marekani, kwa ajili ya kuchunguza chuki dhidi ya Uislamu zinazoenezwa ulimwenguni.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alikuwa mzungumzaji wa kwanza na alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika suala zima la chuki zinazoenezwa dhidi ya Uislamu na wajibu wa dunia nzima kupambana vikali na jambo hilo.

Katika hotuba hiyo, Dk Zarif amesisitizia wajibu wa kutekelezwa ipasavyo malengo ya OIC likiwemo suala zima la Waislamu wa madhehebu yote kuishi pamoja kwa usalama na amani na kuhamasisha mazungumzo yenye manufaa katika ulimwengu wa Kiislamu na baina ya dini na tamaduni tofauti duniani.

Ameongeza kuwa, chuki dhidi ya wageni, dhuki dhidi ya Uislamu, misimamo mikali, taasubu za kimadhehebu, kuendelea kuongezeka ukosefu wa uadilifu na watu wa jamii nyingine kushindwa kuvumilia kuishi na Waislamu na kufanyiwa ukandamizaji wa kila namna Waislamu wa maeneo mbalimbali duniani, zilikuwa ni miongoni mwa mambo muhimu ya kushughulikiwa vilivyo leo hii duniani.

3474277

captcha