Gutteres ameyasema hayo katika tukio la kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi wa rangi iliyofanyika leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, asilimia kubwa ikiwa ni kwa njia ya mtandao.
Guterres amesema “Tunauona ubaguzi ulioenea na kutengwa na kuteswa kwa watu wa asili ya Kiafrika. Tunauona katika dhuluma na ukandamizaji unaovumiliwa na watu wa kiasili na makabila mengine madogo. Tunauona katika maoni yenye kuchukiza ya wanaoona wazungu ni bora zaidi na kwenye vikundi vingine vyenye msimamo mkali. Tunaona pia ubaguzi wa rangi na ubaguzi katika chuki dhidi ya Uyahudi, chuki dhidi ya Waislamu, unyanyasaji wa jamii ndogo za Kikristo na aina zingine za kutovumiliana na chuki dhidi ya wageni. Na tumeuona ubaguzi wa rangi katika vurugu za hivi karibuni za kuchukiza dhidi ya watu wa asili ya Asia, wanaolaumiwa bila haki kwa kusambaza COVID-19.”
Ameongeza kuwa ubaguzi upon a unaendelea kuwepo kwani unashuhudiwa pia katika upendeleo uliojengeka katika kutambua sura na akili bandia.
Katika kusisitiza kuhusu umuhumu wa wanadamu wote kuishi kwa pamoja Gutteres amenukulu sehemu ya aya ya 13 ya Sura Hujurat katika Qur’ani Tukufu isemayo: “. Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane...”