IQNA

Katibu mkuu mpya wa OIC aanza rasmi kazi

11:39 - November 18, 2021
Habari ID: 3474574
TEHRAN (IQNA) Hussein Ibrahim Taha ameanza rasmi kazi kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiisalmu (OIC).

Ameanza kazi rasmi katika sherehe iliyofanyika Jumatano katika makao makuu ya OIC mjini Jeddah Saudi Arabia.

Taha ambaye ni raia wa Chad alichaguliwa kuchukua wadhifa huo  mnamo Novemba 2020 katika Kikao cha 47 za Baraza la Mawaziri wa OIC kilichofanyika Niamey nchini Niger.

Amechukua wadhifa huo katika fremu ya mzunguko wa kijiografia kwa wale wanaochaguliwa katika nafasi ya katibu mkuu wa OIC.  Taha anatazamiwa kubakia katika nafasi hiyo hadi Novemba 2026.

Hussein Ibrahim Taha alizaliwa katika eneo la Abeche nchini Chada mwaka 1951 na baada ya elimu ya msingi na sekondari, mwaka 1972 alielekea Ufarasan katika chuo cha INALCO (Institut national des langues et civilisations orientales).

Aliwahi kuwa balozi wa Chad katika nchi kama vile Ufaransa, Uhispania na Vatican na mwaka 2017 alikuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo na mwaka 2019 aliteuliwa kuwa mshauri wa rais wa Chad. Mwanadiplomasia huyo mwenye uzoefu mkubwa anazunguza lugha za Kiarabu, Kifaransa na Kiingereza.

4014151

Kishikizo: oic CHAD waislamu
captcha