IQNA

22:23 - December 03, 2020
Habari ID: 3473419
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Ufaransa imetangaza mpango mkubwa na ambao haujawahi kushuhudiwa wa kufanya upekuzi katika misikiti ya nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Drmanin amesema mpango huo unaleng akukabiliana na kile alichokitaja kuwa ni ‘misimamo mikali ya kidini’ huku akisema misikiti 76 inashukiwa kueneza itikadi za ‘kujitenga’.

Darmanin ametangaza Alhamisi kuwa, katika siku chache zijazo, kutafanyika upekuzi katika maeneo hayo ya ibada na itafungwa iwapo itabainika kuhusika na uenezaji ‘misimamo mikali’.

Aidha amesema wahajiri 66 wanaoishi ufaransa kinyume cha sheria wanashukiwa kuhusika katika ‘uenezaji misimamo mikali’.

Mwezi uliopita,  ikiwa ni katika kuendeleza kampeni dhidi asasi za Kiislamu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darminian ametangaza mpango wa kupiga marufuku Taasisi ya Kupambana na Chuki Dhidi ya Uislamu au Islamophobia Ufaransa (CCIF).

Mwezi Oktoba, Drmanin alitangaza nia ya kupiga marufuku asasi kadhaa za Kiislamu zisizo za kiserikali nchini humo.

Hayo yanajiri wakati ambao, matamshi ya hivi karibuni ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwamba Uislamu uko kwenye mgogoro duniani kote na msimamo wake wa kuunga makono kitendo kiovu cha jarida la nchi hiyo la Charlie Hebdo cha kuchapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW kimeughadhibisha Ulimwengu wa Kiislamu.

Maandamano makubwa yamefanyika na yanaendelea kufanyika katika nchi mbalimbali kulaani msimamo huo wa Macron. Mbali na maandamano, zinaendeshwa kampeni pia za kususia bidhaa za Ufaransa na sasa kampeni hiyo pia imeenea katika sekta za utamaduni.

3473304

Kishikizo: ufaransa ، waislamu ، macron ، misikiti
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: