IQNA

CAIR kusaidia asasi ya Waislamu Ufaransa ambayo ilifungwa na serikali

12:25 - December 05, 2020
Habari ID: 3473423
TEHRAN (IQNA) -Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR), limetangaza kuwa litatenga s ofisi katika makao makuu yake kwa ajili ya kutumiwa na Taasisi ya Kupambana na Chuki Dhidi ya Uislamu au Islamophobia Ufaransa (CCIF) ambayo imefungwa na serikali ya nchi hiyo.

Katika taarifa, CAIR imesema itatenga nafasi katika makao makuu yake mjini Washington DC kwa ajili ya kutumiwa na Washington DC Taasisi ya Kupambana na Chuki Dhidi ya Uislamu au Islamophobia Ufaransa ilipigwa marufuku na wakuu wa Paris.

Akitangaza kupiga marufuku CCIF, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darminian alidai kuwa asasi hiyo  inaeneza 'propaganda za Kiislamu.'

Hii ni katika hali ambayo CIIF ilianzishwa mwaka 2003 kama asasi isiyo ya kiserikali kwa lengo la kupambana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu Ufaransa.

Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, serikali ya Ufaransa imechukua hatua kadhaa zilizo dhidi ya Waislamu na zinazokiuka uhuru wa kuabudu wa Waislamu wa Ufaransa.

Mwezi Oktoba, Drmanin alitangaza nia ya kupiga marufuku asasi kadhaa za Kiislamu zisizo za kiserikali nchini humo.

Hayo yanajiri wakati ambao, matamshi ya hivi karibuni ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwamba Uislamu uko kwenye mgogoro duniani kote na msimamo wake wa kuunga makono kitendo kiovu cha jarida la nchi hiyo la Charlie Hebdo cha kuchapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW kimeughadhibisha Ulimwengu wa Kiislamu.

Maandamano makubwa yamefanyika na yanaendelea kufanyika katika nchi mbalimbali kulaani msimamo huo wa Macron. Mbali na maandamano, zinaendeshwa kampeni pia za kususia bidhaa za Ufaransa na sasa kampeni hiyo pia imeenea katika sekta za utamaduni.

3473309

 

captcha