IQNA

Arsenal kumtimua mchezaji Muislamu aliyeunga mkono Palestina

17:10 - November 21, 2021
Habari ID: 3474586
TEHRAN (IQNA)- Arsenal ambayo ni Timu maarufu ya Ligi Kuu ya Soka Uingereza (EPL) itamtimua mchezaji Muislamu Mohamed Elneny kutokana na misimamo yake ya kuunga mkono ukombozi wa Palestina.

Gazeti la Misri la Rai Al Youm limeripoti Ijumaa kuwa, Arsenal imetoa taarifa na kusema haitarefusha mkataba wake na Elneny kwa sababau kocha Mikel Areta hamtaki tena katika timu hiyo.

Hatahivyo, vyombo vya habari vimeripoti kuwa Elneny, ambaye ni raia wa Misri, anaadhibiwa kwa sababu ya uungaji mkono wake wa wazi kwa harakati za ukombozi wa Palestina. Aidha baadhi ya duru zikisema uamuzi huo wa Arsenal unafungaamna na uamuzi wa serikali ya Uingereza kutangaza kuwa eti Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ni kundi la kigaidi.

Wakala wa Elbeny, Alaa Nazmi, amesema Arsenal imekataa kurefusha mkataba wa Elneny kutokana na msimamo wake kuhusu kile alichokitaja kuwa ni 'kadhia ya kimataifa'.

Mashabiki wa Elbeny wanasema 'kadhia ya kimataifa' ina maana ya uungaji mkono wa Elneny kwa watu wa Palestina ambao ardhi zao zinakoloniwa na Israel.  Elneny amewahi kutangaza kuwaunga mkono Wapalestina ambao Israel imewatimua kutoka katika nyumba zao katika mtaa wa Sheikh Jarrah mjini Quds (Jerusalem).

Gazeti la Rai Al Youm limeandika kuwa msimamo wa Elbeny umeyakasirisha sana makundi ya Mayahudi nchini Uingereza.

Timu ya Arsenal imewahi kufunga mkataba wa kuupigia debe utawala wa Kizayuni wa Israel ile watalii watembelee ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Kutokana na mkataba huo kulianzishwa kampeni ya kimataifa kususia klabu ya Arsenal . Aliyekuwa kiongozi wa chama cha Leba Uingereza Jeremy Corbyn aliongoza kampeni hiyo ya kutaka Arsenal isusiwe kufuatia mkataba wake huo na utawala wa Israel.

Arsenal pia iliwahi kumkana mchezaji wake wa zamani Muislamu Mesut Ozil aliyetangaza kufungamana na Waislamu waliokuwa wanakandamizwa huko Uighur nchini China.

3476572

captcha