iqna

IQNA

IQNA – Ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu imetoa wito kwa serikali ya Uingereza kuweka mkakati wa kitaifa wa pamoja kupambana na kuongezeka kwa cChuki Dhidi ya Uislamu (Islamophobia), ikionya kuwa mgawanyiko unaozidi katika jamii unadhoofisha imani ya wananchi kwa taasisi za umma na kutishia mshikamano wa kitaifa.
Habari ID: 3480819    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/10

IQNA-Zaidi ya watu mashuhuri 300, wakiwemo waigizaji, wanamuziki na wanaharakati, wametuma barua kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, wakimtaka asitishe uungaji mkono wa Uingereza kwa Israel katika vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3480758    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/30

IQNA – Mwanaume mmoja kutoka mji wa Widnes, Uingereza, amekamatwa na kufunguliwa mashtaka kuhusiana na tukio la wizi katika msikiti wa Warrington.
Habari ID: 3480525    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/11

IQNA – Jumuiya ya Kiislamu ya Altrincham & Hale imetangaza mipango ya kuhamia kutoka eneo lake la sasa kwenye Grove Lane kwenda kwenye Kituo cha Kiislamu na msikiti kilichojengwa mahsusi kwenye Thorley Lane huko Timperley. 
Habari ID: 3480481    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/01

IQNA – Kama miaka iliyopita, tukio la Futari Kubwa litafanyika katika mji wa Bristol, Uingereza, mwaka huu. 
Habari ID: 3480428    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/24

IQNA-Idadi ya matukio na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini Uingereza iliongezeka kufikia kiwango cha juu zaidi mwaka 2024. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na shirika la ufuatiliaji la Tell MAMA, ambalo limesema vita vya Gaza "vimechochea kupita kiasi" masuala ya chuki dhidi ya Waislamu kwenye mitandao ya kijamii.
Habari ID: 3480241    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/19

Haki za Binadamu
IQNA-Kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa Marekani na Uingereza, ripoti ambayo imeandaliwa kwa kutelekeza mswada uliopitishwa na Bunge la Iran mwaka 1391 Hijria Shamsia,
Habari ID: 3479910    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/16

IQNA - Kulingana na data ya hivi punde kutoka Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa Uingereza (ONS), Muhammad limekuwa jina la mtoto maarufu zaidi la wavulana England na Wales mnamo 2023.
Habari ID: 3479867    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/06

Waungaji Mkono Palestina
IQNA - Mji mkuu wa Uingereza,  London siku ya Jumamosi ulikuwa eneo la mjumuiko mkubwa ulioandaliwa na waandamanaji wanaounga mkono Palestina.
Habari ID: 3479840    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/02

Qiraa
IQNA - Qari wa Misri Ahmed al-Sayyid al-Qaytani alishika nafasi ya kwanza katika kategoria ya qiraa au usomaji Katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Uingereza wiki iliyopita.
Habari ID: 3479717    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/08

Mashindano ya Qur'ani
IQNA - Sherehe imefanyika nchini Uingereza kutangaza na kuwatunuku washindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3479711    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/06

Michezo
IQNA - Chama cha Soka cha Uingereza (FA) kimeomba msamaha kwa mwanasoka mwanamke mwenye uraia pacha wa Uingereza - Somalia.
Habari ID: 3479684    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/02

Watetezi wa Palestina
IQNA – Madiwani 114 wa Muslim wa chama tawala cha Leba Uingereza wamemuandikia barua Waziri Mkuu wa Uingereza, wakitaka kuwekewa vikwazo vya mara moja vya silaha dhidi ya Israel huku vikosi vya utawala huo vikiendelea kutumia silaha na zana za viita  zinazotolewa na nchi za Magharibi kutekeleza mauaji ya kimbari huko Palestina na Lebanon.
Habari ID: 3479611    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/18

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA – Ripoti ya Ofisi ya Mambo ya Ndani Uingereza imefichua ongezeko la karibu 40% ya vitendo vya chuki za kidini huwa zinawalenga Waislamu katika maeneo ya England na Wales.
Habari ID: 3479579    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/12

Waislamu Uingereza
IQNA - Takriban mashirika 80 ya Kiislamu na viongozi wa jamii za Waislamu wametoa wito kwa serikali ya Uingereza kuchukua hatua madhubuti ili kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Habari ID: 3479352    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/30

Waislamu Uingereza
IQNA -Kuna wasiwasi unaoongezeka miongoni mwa Waislamu wa Uingereza kuhusu usalama wao baada ya ghasia za hivi majuzi nchini humo.
Habari ID: 3479295    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/18

Waislamu Uingereza
IQNA - Mwanamume mmoja amerekodiwa kwenye video akirusha maneno ya chuki dhidi ya Uislamu na kumtemea mate dereva wa basi Muislamu mjini London huku kukiwa na ongezeko la ghasia dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya.
Habari ID: 3479249    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/09

Machafuko Uingereza
IQNA: Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Yvette Cooper, siku ya Jumatatu alibainisha chuki dhidi ya Uislamu kama kichocheo cha ghasia za hivi karibuni za wazungu wenye misimamo mikali wa mrengo wa kulia katika miji kadhaa, ambayo imesababisha uharibifu mkubwa na karibu watu 400 kukamatwa.
Habari ID: 3479237    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/06

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA – Tukio la Muislamu kudungwa kisu katika kituo cha treni cha Blundellsands & Crosby huko Liverpool limeacha jamii ya Waislamu wa jiji hilo katika mshtuko huku Waislamu kote Uingereza sasa wanahofia usalama wao huku kukiwa na maandamano ya magenge ya watu wenye misimamo mikali ya chuki ya mrengo wa kulia.
Habari ID: 3479222    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/03

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA - Vichwa vitatu vya nguruwe vimepatikana nje ya shule mbili na kituo cha vijana huko Rainham, Uingereza vikiambatana na maandishi ya chuki dhidi Uislamu.
Habari ID: 3479192    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/27