Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kuwait,KUNA, waumini wanaoingia misikitini sasa wanatakiwa kutokaribiana, wavae barakao na kila moja abebe mkeka binafsi wa kusali.
Aidha ni sharti kubakia wazi madirisha na milango wakati wote wa sala na hotuba.
Aidha katika vikao vya kusajili ndoa au nikah ni watu sita tu wataruhusiwa kushiriki kuanzia Januari 9.
Halikadhalika serikali imepiga marufuku mijumuiko yote katika maeneo ya umma kuanzia Januari 9 hadi Februari 28.
Siku ya Jumatano Kuwait ilisajili kesi 2,413 mpya za COVID-19 na kwa msingi huo hadi sasa watu 425, 455 wameambukizwa nchini humo huku waliofariki kutokana na ugonjwa huo wakiwa ni 2,469.