IQNA

Kuwait yaruhusu tena darsa za Qur’ani msikitini

19:18 - November 05, 2021
Habari ID: 3474519
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Kuwait imetangaza kuwa darsa za Qur’ani na kidini pamoja na harakati nyingine za kiutamaduni zitaruhusiwa tena ndani ya misikiti.

Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Issa Ahmad Mohammad Hassan Al-Kandari ametoa taarifa na kusema misikiti yote Kuwait ina ruhusa kuanzisha tena darsa za Qur’ani, harakati za kiutamaduni na mafunzo ya kidini kwa kuhudhuria ana kwa ana.

Misikiti ya Kuwait ilisimamisha shughuli zote zaidi ya miezi 18 iliyopita kutokana na janga la COVID-19.

Waziri Al Kandari amesema misikiti itatakiwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea COVID-19 ikiwa ni pamoja na na kuvaa barakoa na kutokaribiana.

Misikiti imefunguliwa tena kikamilifu nchini Kuwait baada ya serikali ya nchi hiyo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi kufanikiwa kudhibiti maambukizi ya COVID-19. Nchi zingine za Kiarabu ambazo zimechukua maamuzi kama hayo ya Kuwait ni pamoja na Qatar, Algeria na Misri.

3476340

captcha