Ensaiklopidia hiyo ni seti na majmui ya vitabu vinavyotoa maelezo kuhusu maeneo ya kijografia yaliyomo ndani ya sura za Qur'ani Tukufu.
Mtayarishaji wa ensaiklopidia hiyo Muhammad Hassan Arab ameandika katika utangulizi wake kuwa lengo la tabu hilo kubwa ni kutoa maelezo na ufafanuzi kuhusu maeneo ya kijiografia yaliyotajwa au kuashiriwa katika aya za Qur'ani ili watafutaji wa elimu na maarifa na watafiti wa masuala ya Qur'ani waweze kuelewa habari za maeneo hayo kwa wepesi.
Ensaiklopidia hiyo inaarifisha na kutoa ufafanuzi wa maeneo 160 ya kijografia yaliyotajwa katika aya mbalimbali za Qur'ani.
Katika kitabu hicho mwandishi ametumia mbinu ya kutoa maelezo kuhusu maana ya kilugha ya neno linalochunguzwa ambalo linaashiria eneo makhsusi la kijografia, kisha anaeleza mipaka ya kijografia ya eneo hilo kwa kutegemea Qur'ani Tukufu na mipaka yake ya sasa. 400030