Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA tawi la kusini-mashariki mwa Asia, nuskha hizo za Quran zimesambazwa huko India, Indonesia, Bangladesh, Malaysia na Ufilipino. Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quran imesema lengo lengo kuu la usambazaji huo ni kuhakikisha wanafunzi katika Madrassah na Misikiti wana Misahafu ya kutosha.
Wakati huo huo Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quran imetangaza kuwa imesambaza Misahafu mingine huko Afrika Kusini, Somalia, Tanzania, Visiwa vya Comoro, Sudan, Ethiopia, Nigeria, Uganda, Jordan, Ufaransa, Bulgaria, Bosnia Herzegovina na Tatarstan.
Jumuiya hiyo imesema idadi ya Misahafu iliyotumwa katika nchi hizo ni karibu lefu 93.
407055