IQNA

Mkutano wa 'Taathira ya Qur'ani katika Jamii za Kiislamu' wafanyika Nigeria

15:30 - July 04, 2009
Habari ID: 1798351
Mkutano wa siku tatu uliojadili taathira za Qur'ani Tukufu katika maendeleo ya mwanadamu na jamii za Kiislamu ulimaliza shughuli zake jana katika mji wa Lagos nchini Nigeria.
Mkutano huo ulisimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu na Chuo cha Kimataifa cha Elimu ya Qur'ani cha Ghana.
Wataalamu waliohudhuria mkutano huo walijadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbinu mbalimbali za elimu ya tajwidi na tafsiri ya Qur'ani.
Chuo cha Sayansi ya Qur'ani cha Ghana ndio chuo kikubwa zaidi cha taaluma hiyo huko Magharibi mwa Afrika na kila mwaka hupokea wanafunzi kutoka nchi jirani za eneo hilo. 429238

captcha