IQNA

"Quran, Kitabu cha Maisha" ndio nara ya Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Quran Tukufu

13:01 - July 25, 2010
Habari ID: 1961832
Baraza la Sera la Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Quran Tukufu limetangaza kuwa: "Qur'an Kitabu cha Maisha" ndio nara ya maonyesho ya mwaka huu yatakayofanyika mjini Tehran.
Ripota wa Shirika la Habari la Quran IKNA amenukulu Idara ya Masuala ya Umma ya Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Quran Tukufu ikitangaza nara hiyo ya "Quran, Kitabu cha Maisha" katika kikao cha Baraza la Sera la maonyesho hayo. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Dr. Sayyed Mohammad Husseini.
Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Quran Tukufu yatafanyika Tehran kuanzia tarehe 27 Shaaban hadi tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
620987
captcha