IQNA

Waturuki wanunua kwa wingi Qur'ani wakijitayarisha kwa mwezi wa Ramadhani

19:33 - August 05, 2010
Habari ID: 1967692
Ununuzi wa kitabu kitakatifu cha Qur'ani umeshamiri zaidi katika maduka ya kuuza vitabu nchini Uturuki katika siku hizi za kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani, kiasi kwamba kitabu hicho kinashika nafasi ya kwanza katika orodha ya vitabu vilivyonunuliwa kwa wingi zaidi katika wiki hii.
Gazeti la Zaman la Uturuki limepripoti kuwa katika kipindi hiki cha kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani, maduka makubwa ya kuuza vitabu ya NT yamekuwa yakiuza nakala 35 hadi 50 za kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa siku.
Gazeti la Zaman limemnukuu Mustafa Unal ambaye ni mmoja wa maafisa wa maduka hayo akisema kuwa kutokana na watu wengi kuvutiwa mno na chapa mpya ya Qur'ani, imeundwa kamati iliyopewa jina la "Kamati ya Kutoa Zawadi Qur'ani" na kwamba watu wanaweza kununua nakala kadhaa za kitabu hicho na kuzigawa kama zawadi katika misikiti na vituo vya Kiislamu. Mustafa Unal ameongeza kuwa bei ya vitabu mwaka huu imepungua kwa kiasi kikubwa suala ambalo limewahamasisha wananchi kusoma na kununua kwa wingi vitabu. 626630

captcha