Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai Ibrahim Bu Malha amesema kuwa wasomi 28 watahutubia katika monyesho hayo wakizungumzia maudhui mbalimbali zinazohusiana na taaluma ya Qur’ani. Bu Malha amesema kuwa hotuba 25 zitatolewa kwa lugha ya Kiarabu na wazungumzaji wengine watatoa hotuba zao kwa lugha za Malay na Bangla.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai ameongeza kuwa hotuba hizo zitatolewa katika vituo mbalimbali mjini Dubai. Amesema kuwa Imamu wa msikiti wa al Aqsa huko Palestina pamoja na mashekhe kutoka nchi za Syria, Saudi Arabia, Misri na Ufaransa watahutubia vikao hivyo. 627759