Nakala za kitabu kitukufu cha Qur'ani zilizotarjumiwa kwa lugha za Kifaransa, Kihispania na Kitamazight (lugha ya Mabarbari wa kaskazini mwa Afrika) zimesambazwa katika misikiti, vituo vya kuhifadhisha Qur'ani ma jumuiya za masuala ya kheri na utamaduni za Algeria.