Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa jarida la Nurul Yaqin linachapishwa kwa lugha ya Kiarabu.
Miongoni mwa maudhui zilizojadiliwa katika toleo la kwanza la Nurul Yaqin ni Kutakasa Nafsi katika Mtazamo wa Qur'ani Tukufu, Sifa Makhsusi za Mtume Muhammad (saw) katika Qur'ani na Suna, Uchunguzi Kuhusu Kuwapenda Ahlul Bait (as) katika Qur'ani na Mfungamano Uliopo kati ya Qur'ani na Sahifa Sajjadiyya.
Mambo mengine yaliyochunguzwa katika jarida hilo ni kuoanisha kati ya hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Imam Ja'far Sadiq (as) na aya za Qur'ani Tukufu, uchunguzi wa matatizo ya ndoa na familia kwa mujibu wa Qur'ani na Suna za Mtume na utafiti kuhusu Risala ya Haki ya Imam Zainul Abidin (as).
Toleo la kwanza la jarida la Nurul Yaqin limewekwa katika chumba cha Ivory Coast katika maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani yanayoendelea mjini Tehran. 629185