IQNA

Kikao cha kuchunguza muundo wa Sura za Qur'ani chafanyika Saudia

13:27 - August 12, 2010
Habari ID: 1971813
Jumuiya ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Sihat nchini Saudi Arabia itaandaa kikao cha kuchunguza muundo na kalibu jumla ya sura za Qur'ani Tukufu.
Kikao hicho ambacho kimeandaliwa kwa ajili ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wa mji huo kitafanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kitaendelea kwa muda wa siku tano.
Jumuiya ya Qur'an ya mji wa Sihat imetoa tangazo la kuwaomba wanaotaka kushiriki katika kikao hicho kujiandikisha. Kikao hicho kitaendeshwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Helad as-Suyud ambaye ni kati ya wanazuoni wa ngazi za juu wa Qur'ani Tukufu katika jamii ya Mashia nchini Saudia.

631305




captcha