Msimamizi wa chumba cha Ivory Coast katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran Abdullah Dosou ambaye pia ni mwanafunzi wa taaluma ya falsafa katika Chuo Kikuu cha al Mustafa al Alamiyya amesema wasanii hodari wa Ivory Coast wanabuni michoro mbalimbali na kuandika aya na sura za Qur'ani juu yake kwa kutumia hati nzuri na za kuvutia. Amesema kuwa mfano wa sanaa hiyo ni mchoro wa tembo unaaonyeshwa sasa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran ambao umetengenezwa na wasanii wa Ivory Coast na kuandika aya za suratul Fiil juu yake kwa kutumia hati nzuri na za kuvutia.
Chumba cha Ivory Coast katika maonyesho ya Tehran kinajumuisha pia vitabu na makala zilizoandikwa na wasomi mbalimbali kuhusu taalumu ya Qur'ani Tukufu.
Chumba hicho pia kina michoro na picha za mashindano ya Qur'ani nchini Ivosry Coast, sherehe za kuhitimisha na kufasiri Qur'ani, picha za misikiti ya kale, ibada ya Lailatul Qadr na kadhalika. 631373