IQNA

0810 Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Kusoma na kuhifadhi Qur'ani kunapaswa kuwa utangulizi wa kufahamu maarifa ya kitabu hicho na kuyafanyia kazi

10:20 - August 13, 2010
Habari ID: 1972209
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa ustawi unaoendelea kila siku wa kupewa mazingatio Qur'ani katika jamii hususan kati ya mabarobaro na vijana ni neema kubwa ambayo huenda haiwezi kulinganishwa na neema nyingine yoyote.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyasema hayo jana jioni katika siku ya kwanza ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika hadhara kubwa ya makari bora wa Qur'ani, walimu na mahafidhi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu kutoka maeneo mbalimbali ya Iran.
Makari kadhaa walisoma Qur'ani Tukufu katika majlisi hiyo ambayo iliendelea kwa kipindi cha masaa manne.
Amesema majlisi hii ina tamu ya aina yake na taathira kubwa na akaongeza kuwa kusoma na kuhifadhi Qur'ani kunapaswa kuwa utangulizi wa kufahamu maarifa ya kitabu hicho na kuyatendea kazi.
Ayatullah Khamenei amesisitiza pia juu ya udharura wa kuthaminiwa mwenendo unaokua kila siku wa watu kuipenda na kuelekea kwenye Qur'ani katika jamii na akasema kuifahame vyema Qur'ani ni sharti la kuweza kufaidika na maarifa ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewausia makari na mahafidhi wa Qur'ani kujua vyema tarjumi ya kitabu hicho na akaongeza kuwa maarifa ya Qur'ani kwa hakika ni darsa ya maisha na kuwa na uwezo mkubwa wa kutarjumi Qur'ani humuwezesha mtu kufahamu maana na maarifa ya kitabu hicho.
Mwishoni mwa majlisi hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliongoza sala za Magharibi na Ishaa na hadhirina wakapata futari na pamoja na Ayatullah Ali Khamenei. 631958





captcha