IQNA

Utekelezaji wa ratiba maalumu ya al Rauhu wal Rayhan katika kituo cha Qur’ani cha Bibi Ruqayyah (as)

11:37 - August 14, 2010
Habari ID: 1972747
Kituo cha Qur’ani cha Bibi Ruqayyah (as) kimeanza kutekeleza ratiba maalumu ya kisomo cha Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyopewa jina la al Rauhu wal Rayhan.
Ratiba hiyo ya al Rauhu wal Rayhan inayotekelezwa katika usiku za mwezi huu mtukufu inajumuisha kazi za kusahihisha kiraa za Qur’ani, mahfali za Kiqur’ani, qasida za Kiislamu, mafunzo ya kaligrafia ya Kiislamu na kukutana na walimu wa Qur’ani.
Kituo hicho pia kinatoa mafunzo ya tajwidi ya Qur’ani makhsusi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Kituo cha Qur’ani cha Bibi Ruqayyah (as) kinachoongozwa na Abdul Jalil al Makrani wa Saudi Arabia kiko katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran na kinatoa mafunzo ya kitabu kitukufu cha Qur’ani kwa wanafunzi wa kigeni. 632526


captcha