IQNA

Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kwa walemavu wa akili yafanyika Misri

12:04 - August 17, 2010
Habari ID: 1975244
Awamu ya kwanza ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu maalumu kwa walemavu wa akili yalianza siku ya Jumapili huko Cairo mji mkuu wa Misri.
Mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri. Kwa mujibu wa gazati la nchi hiyo la al-Yaum as-Sabi', mashindano hayo ambayo yanafanyika katika ukumbi wa wizara iliyotajwa yanafanyika katika hatua tatu za kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi juzuu 10 na kuhifadhi juzuu moja ya kitabu hicho kitakatifu.
Mashindano hayo yamepangwa kumalizika kesho Jumatano. Awali Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri ilitangaza kwamba hayo ni mashindano ya kwanza ya aina yake kuwahi kufanyika duniani na kwamba ina lengo la kuyafanya kuwa ya kimataifa. 634369
captcha