IQNA

Mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani yaanza nchini Yemen

12:04 - August 17, 2010
Habari ID: 1975247
Mashindano ya 14 ya kimataifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu yameanza leo Jumanne katika mkoa wa Umran nchini Yemen.
Kwa mujibu wa tovuti ya at-Thaura, mashandano hayo ambayo yamedhaminiwa na Idara ya Wakfu na Muongozo wa Kiislamu ya Yemen yanawashirikisha washindani 56 wa kike na kiume na kwamba watashindana katika hatua mbili za kuhifadhi na kusoma kitabu hicho kitakatifu.
Waandaaji wa mashindano hayo wanasema kuwa lengo la kufanyika kwake ni kuwashajiisha vijana wahifadhi na kusoma Qur'ani, suna za Mtume (SAW) pamoja na kuimarisha misimamo na mielekeo ya wastani na ya umoja wa Kiislamu miongoni mwao.
Ahmad Swalih as-Shamuri mmoja wa wasimamizi hao katika mkoa wa Umran amesema kuwa mashindano ya Qur'ani ni hatua muhimu katika kulinda utambulisho wa Kiislamu na umoja wa umma wa Kiislamu mkabala na mielekeo ya kufurutu ada na vilevile misimamo mikali na ya taasubi. Amesisitiza juu ya umuhimu wa kuhifadhiwa Qur'ani na kutekelezwa mafundisho na thamani zake za kidini katika maisha ya kila siku ya Waislamu. 635184
captcha