IQNA

Nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu zagawanywa kwa wanaozuru al Kaaba

12:37 - August 17, 2010
Habari ID: 1975399
Ofisi ya Mkuu wa Jumuiya ya Misiki nchini Saudi Arabia imetangaza kuwa nakala milioni moja za kitabu kitukufu cha Qur'ani zinagawanywa kwa watu wanaozuru nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu katika Masjidul Haraam ikiwa ni sehemu ya mpango wa kudhamini mahitaji ya watu wanaozuru na kutekeleza ibada ya sala katika msikiti huo.
Gazeti la Arab News limeandika kuwa Jumuiya ya Misikiti ya Saudia imetangaza kuwa nakala hizo milioni moja za kitabu kitukufu cha Qur'ani zimechapishwa na Taasisi ya Uchapishaji ya Mfalme Fahad mjini Madina kwa viwango na saizi tofauti.
Mkuu wa jumuiya hiyo ameongeza kuwa nakala hizo zinajumuisha tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha 12 tofauti kikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kiurdu, Kituruki na Kihispania na nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za braille (makhsusi kwa ajili ya wasioona). Amesisitiza kuwa mpango huo unatekelezwa ili kuwawezesha wageni na watu wasioona kufaidika na kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Jumuiya ya Misikiti ya Saudi Arabia imetangaza kwamba nakala hizo zimewekwa katika pembe mbalimbali za Masjidul Haraam ili watu wanaozuru al Kaaba na wanaoenda kusali waweze kuzitumia kwa wepesi. 635209
captcha