Kwa mujibu wa tovuti ya ICCUK mashindano hayo yanafanyika kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha London kwa shabaha ya kuwashajiisha vijana wa Kiislamu wahifadhi na kusoma Qur'ani, washiriki katika mashindano ya Qur'ani, shughuli za Kiislamu na kuwafanya wayatekeleze mafundisho ya kitabu hiki kitakatifu katika maisha yao ya kila siku. Mashindano hayo yatafanyika katika makundi matano ya kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 20, juzuu 10, juzuu 5 na hatimaye juzuu moja ya Qur'ani. Mashindano hayo ambayo yatawashirikisha vijana wa Uingereza walio na umri wa chini ya miaka 25 hayatazingatia umri wa washindani chini ya umri huo ulioainishwa.
Mashindano hayo yatasimamiwa na kutathminiwa na marefa ambao ni wasomaji mashuhuri wa Qur'ani kutoka Misri pamoja na maimamu wa Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha London.
Washindi wa mashindano hayo watashukuriwa na kupewa zawadi na kituo kilichotajwa cha utamaduni wa Kiislamu na vilevile Msikiti Mkuu wa London mwishoni mwa mwezi wa Ramadhani. 63576