Kwa mujibu wa tovuti ya jumuiya hiyo ya Kiislamu, dua ya Iftitaah imekuwa ikisomwa kila usiku kuanzia saa mbili, mara tu baada ya kuswaliwa swala za Maghrib na Ishaa. Baada ya kufuturu pia kunakuwa na kikao cha kujibu maswali mbalimbali yanayoulizwa na washiriki. Wanazuoni wawili kutoka Lebanon ndio wanaojibu maswali hayo.
Vilevile Kituo cha Kiislamu cha Zeinab katika eneo la Courneuve kimekuwa kikitekeleza ratiba maalumu za mwezi wa Ramadhani. Ratiba hizo ni pamoja na kusoma Qur'ani, dua ya Iftitaah na dua ya Kumeil katika usiku wa kuamkia Ijumaa.
Ratiba nyingine ni kutoa futari na kuandaa darasa maalumu za kidini katika mwezi huu. 635699