Vipindi hivyo vya Qur'ani vimekuwa vikimshirikisha Sheikh Faisal al-Awami, mmoja wa maulama na wanazuoni mashuhuri wa Kishia kutoka katika mji wa Qatif nchini Saudi Arabia na vimekuwa vikitangazwa hewani saa mbili na nusu usiku kwa wakati wa Bahrain.
Vipindi hivyo ambavyo vitaendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Ramadhani vimeteyarishwa kwa lengo la kuimarisha mafundisho ya kimaanawi na Qur'ani miongoni mwa waumini wa Kiislamu.
Televisheni ya Fourteen ambayo imepewa jina hilo kutokana na maasumu watoharifu 14 wa Kiislamu ina lengo la kueneza mafundisho na fikra za kidini na kiutamaduni za Ahlul Beit (AS). Televisheni hiyo ilianzishwa hivi karibuni na Mashia wa Bahrain na imekuwa ikipeperusha hewani vipindi mbalimbali vya kidini, kitamaduni na Qur'ani katika mwezi huu mtukufu. 637366