Kanisa na mji wa Jacksonville katika jimbo la Florida ambalo limeitangaza siku ya tarehe 11 Septemba kuwa ni siku ya kuchomwa moto Qur'ani, limewaandikia barua viongozi wa serikali ya jimbo hilo likiwataka waruhusu kitendo hicho cha kuchomwa moto hadharani kitabu cha Mwenyezi Mungu. Ombi hilo limepingwa vikali na viongozi hao.
Viongozi wa jimbo la Florida pia wamesema kuwa iwapo Qur’ani itachomwa moto hadharani kanisa la Jacksonville litalazimishwa kulipa faini na viongozi wake watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Jumuiya na makundi ya Kiislamu katika nchi mbalimbali za Kiislamu yametangaza upinzani wao mkali dhidi ya kitendo hicho cha kukivunjia heshima kitabu cha Mwenyezi Mungu na wamewataka viongozi wa kanisa hilo kujiepusha na kitendo hicho. 637892