IQNA

Kubainishwa nafasi ya Mashia na Wairani katika kueneza tafsiri na mafundisho ya Qur'ani

12:36 - August 24, 2010
Habari ID: 1979994
Nafasi muhimu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Wairani katika kueneza tafsiri na mafundisho ya Qur'ani Tukufu imebainishiwa wageni wanaoyatembelea Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran.
Ubainishaji huo unafanyika kupitia lugha mbili za Kifarsi na Kiingereza kwa kutegemea hoja na dalili za kihistoria. Kwa mujibu wa shirika la habari la Iqna kutoka katika maonyesho hayo, ubainishaji huo unatimia kupitia jedwali na chati zilizotayarishwa na Taasisi ya Tarjumi ya Wahyi (Qur'ani) na kwa kutegemea vyanzo vya kuaminika vya utaalamu wa vitabu na maisha ya wasomi na maulamaa. Chati hizo zinawagawa katika makundi tofauti ya tafsiri na masomo mengine ya Qur'ani Tukufu wanazuoni na maulamaa wa Kiirani na Kishia waliohudumia kwa uwezo wao wote kitabu hiki kitakatifu.
Wasomi na maulama hao wa Kiirani wanaonyeshwa katika chati hizo bila kujali madhehebu zao za Shia na Suni.
Maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yataendelea hadi Ijumaa tarehe 3 Septemba. 640024
captcha