Mashindano hayo yamekuwa yakifanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kitaifa cha Utamaduni cha vijana wa mji huo, ikiwa ni katika utekelezwaji wa ratiba maalumu za kila mwaka za kituo hicho katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumzia suala hilo, Abdullah Abdul Ilah Salim, Mkurugenzi wa kituo hicho amesema kuwa huu ni mwaka wa saba ambapo kituo hicho kinaandaa mashindano hayo na kwamba katika miaka iliyopita zaidi ya wahifadhi Qur'ani 500 wamekuwa wakishiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani.
Amesema mashindano hayo yanafanyika kwa shabaha ya kuhudumia Qur'ani na kuimarisha uwezo wa wanawake katika kuhifadhi Qur'ani na kutumia vyema vipawa na vipaji vyao katika uwanja huo. Washiriki wa mashindano hayo wameshindana kuhifadhi juu 15 za Qur'ani. 640400