Ibadullah Ramadhani ameliambia shirika la habari za Qur'ani la kimataifa IQNA kwamba sherehe za kuanza ujenzi wa kituo hicho kikubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu cha Qur'ani ambacho kimepewa jina la 'Tehran Saraye Qur'ani' kwa maana ya Tehran, Nyumba ya Qur'ani, zinafanyika hii leo. Kituo hicho kinajengwa katika ardhi yenye ukubwa wa hektari 60.
Ameongeza kuwa sherehe hizo zitahudhuriwa na Meya wa jiji la Tehran Muhammad Baqir Qaliibaf na viongozi wengine wa serikali na jeshi la Iran.
Meya wa jiji la Tehran atahutubia sherehe hizo akieleza shughuli za kiqur'ani zilizofanywa na Halmashauri ya Jiji la Tehran.
Mradi huo mkubwa wa Kiislamu utakamilika katika kipindi cha miaka minne ijayo. 640215