IQNA

Mkutano wa Kuwa Karibu na Qur'ani Tukufu wafanyika al Awamiya Saudi Arabia

13:53 - August 26, 2010
Habari ID: 1981538
Mkutano wa kila mwaka wa kuwa karibu na Qur'ani Tukufu umefanyika katika mji wa al Awwamiyya wenye idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kikao hicho cha kusoma Qur'ani Tukufu iliyopita kimehudhuriwa na makari maarufu wa eneo la Qatif nchini Saudi Arabia. Hafla hiyo ya Qur'ani imefanyika katika fremu ya tamasha ya kiutamaduni ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa himaya ya kamati ya utamaduni ya Jumuiya ya al Salam ya al Awwamiyya.
Mkutano wa kila mwaka wa kuwa karibu na Qur'ani Tukufu umekuwa ukifanyika katika eneo hilo la Saudi Arabia lenye idadi kuwa ya Mashia kwa zaidi ya miaka 18 sasa.
Wakati huo huo Taasisi ya Sayansi za Qur'ani ya Darul Qur'an katika mji wa al Emran katika mkoa wa al Ahsa wenye Mashia wengi nchini Saudi Arabia Ijumaa iliyopita iliandaa mkutano wa kuwa karibu na Qur'ani Tukufu katika ukumbi wa “Husseiniya al Muhamadiyya” katika mji huo.
641523
captcha