Kwa mujibu wa gazeti la Kuwait la ar-Rai mashindano hayo yameandaliwa na Sekritarieti ya Mashindano ya Qur'ani ya Tuzo ya al-Kharafi ya Misri, na washindi wa mwisho watapewa zawadi ya lira ya Misri ya 220,000.
Ibrahim Swalih, mkuu wa jumuiya ya al-Kharafi na msimamizi wa mashindano hayo, amesema kuwa yamefanyika katika makundi mawili ya watoto wadogo na vijana. Amesema, kamati inayosimamia mashindano hayo pia ina mpango wa kuchapisha vitabu vya mafunzo ya kuhifadhi, kusoma na kuandika Qur'ani Tukufu kwa maandishi ya mkono na kuvisambaza miongoni mwa watu walio na hamu ya kujishughulisha zaidi na masuala ya Qur'ani. 641554