IQNA

Uturuki kuwa mwenyeji wa kongano la kimataifa la Mwaka wa 1400 wa Kuteremshwa Qur'ani Tukufu

12:36 - August 28, 2010
Habari ID: 1982575
Kongamano la kimataifa la Mwaka wa 1400 wa Kuteremshwa Qur'ani Tukufu limepangwa kufanyika Jumapili ya tarehe 5 Oktoba mjini Istanbul Uturuki chini ya usimamizi wa kituo cha Utafiti, Utamaduni, Sanaa na Historia ya Kiislamu cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC.
Kongamano hilo la kimataifa litahudhuriwa na zaidi ya shakhsia 80 wa ngazi za juu wa kidini na kisiasa, wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za Kiislamu na wataalamu wa masuala ya Kiislamu kutoka nchi 40 duniani. Vilevile maafisa wa balozi wa kigeni nchini Uturuki wamealikwa katika kongamano hilo.
Mkuu wa kituo hicho Halit Eren amesema kuwa katika kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiislamu kilichofanyika miezi kadhaa iliyopita nchini Tajikistan, Uturuki ilitoa rasmi pendekezo la kutangazwa mwaka 2010 kuwa mwaka wa Qur'ani na kuzitaka nchi zilizohudhuria kikao hicho kuipa kipaumbele Qur'ani katika ratiba zao za mwaka 2010 na 2011. Amesisitiza kuwa pendekezo hilo lilikubaliwa na nchi zilizohudhuria kikao hicho.
Halit Eren amesema kuwa miongoni mwa ajenda za kongamano hilo la Mwaka wa 1400 wa Qur'ani Tukufu ni kuweka ratiba za shughuli za kidini kwa mujibu wa mahitaji ya nchi mbalimbali na kuchunguza suhula zilizopo kwa ajili ya kueneza utamaduni wa Qur'ani duniani. 642520


captcha