IQNA

Wairani waishio Tanzania wahudhuria kisomo cha Qur’ani

2:16 - August 30, 2010
Habari ID: 1983953
Wairani wanaoishi katika mji wa Dar es Salaam nchini Tanzania wanahudhuria kisomo cha Qur’ani kila usiku katika ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu mjini humo.
Wairani hao husikiliza kiraa ya Zamanlou, msomaji wa kimataifa wa Irani alietumwa nchini humo katika mwezi huu wa Ramadhani.
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania Mustafa Ranjbar ameliambia Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa IQNA kwamba Wairani waishio mjini Dar es Salaam wamekuwa wakihudhuria vikao vya kiraa ya Qur’ami saa mbili na nusu hadi tano usiku kila siku katika ubalozi wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Ranjab ameongeza kuwa Wairani hao pia husoma dua ya Iftitah na juzuu moja ya Qur’ani Tukufu chini ya usimamizi wa msomaji wa kimataifa wa Qur’ani kutoka Iran.
Ameongeza kuwa ratiba nyingine ya vikao hivyo ni hotuba za viongozi wa kidini ambao hutoa mawaidha kuhusu utukufu wa mwezi wa Ramadhani na kufafanua sheria za kifikhi.
Programu hiyo ya kisomo cha Qur’ani ambayo pia inahudhuriwa na mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu nchini Tanzania itaendelea hadi mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. 644068
captcha