IQNA

Kumalizika mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani nchini India

12:23 - August 31, 2010
Habari ID: 1984989
Mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu yalimalizika siku ya Jumapili huko Bombay nchini India.
Kwa mujibu wa tovuti ya UMMID, mashindano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Aqdas na kamati ya Aman ambayo yote mawili ni mashirika yasiyo ya kiserikali, katika Nyumba ya Hija iliyoko katika mji huo. Washiriki 236 ambao wote ni wanafunzi wa madrasa na taasisi za Kiislamu katika jimbo la Maharashtra walishiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika katika makundi mawili ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani.
Mashindano hayo ambayo ni moja ya mashindano makubwa zaidi nchini India yameandaliwa kwa muda wa siku tatu na yamefanyika kwa mujibu wa ratiba maalumu ya shughuli za mwezi wa Ramadhini chini ya anwani ya Sherehe ya Kuteremshwa Qur'ani.
Marefa 16 wa mashindano hayo waliwachagua washindi watatu kutoka katika kila kundi na kupewa zawadi kutokana na juhudi walizofanya katika usomaji na uhifadhi wa Qur'ani.
Katika hatua ya mwanzo, wahifadhi na wasomaji bora wa Qur'ani wapatao 50 walichaguliwa katika mashindano ya awali na kuruhusiwa kuingia katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo iliyokamilika siku ya Jumapili. Baada ya kumalizika mashindano hayo, wasimamizi wamechukua uamuzi wa kuyaandaa kila mwaka katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. 644905
captcha