Tafsiri hizo ni kiunganishi muhimu cha dini na maisha ya mwanadamu. Akizungumzia suala hilo Mahdi Firouzon, mkuu wa Taasisi ya Imam Sadr amesema kuwa kati ya vitabu vyote alivyoandika kuhusiana na maarifa ya dini na Uislamu, tafsiri alizoandika kuhusiana na Qur'ani ni jambao linalomvutia zaidi msomaji wa vitabu vya mwanazuoni huyo mashuri wa Kiislamu. Amesema Imam Musa Sadr alijishughulisha zaidi na tafsiri za sura fupi za Qur'ani au akichukua mjumuiko fulani wa aya za Qur'ani na kisha kuzitafsiri kwa manufaa ya wasomaji.
Tafsiri hizo za aya za Qur'ani ni zile alizokuwa akizitoa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani au katika hutuba zake fupi alizotoa kwa minasaba mbalimbali zilizochukua muda wa dakika kumi kwa kawaida na kutangazwa kwenye redio ya Lebanon. Kwa msingi huo mwanazuno huyo hana tafsiri kamili ya Qur'ani Tukufu. Tafsiri za Imam Sadr zimesimama juu ya msingi wa thamani za kiutu na maadili bora ya mwanadamu. 646394