IQNA

Waislamu wa Afghanistan watoa wito wa kutetewa Qur'ani Tukufu

17:35 - September 07, 2010
Habari ID: 1989962
Mamia ya wananchi wa Afghanistan wamemiminika mabarabarani kulalamikia kitendo cha Marekani cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu. Waandamanaji hao wametoa wito wa kulindwa Qur'ani Tukufu mbele ya mashambulizi ya maadui
Waandamaji hao walikuwa wakipiga nara na kutoa kaulimbiu za "Mauti kwa Marekani" kufuatia kanisa moja la Marekani kusisitizia tena nia yake ya kuchoma Kitabu Kitakatifu cha Qur'ani katika maadhimisho ya Septemba 11.
Watu muhimu wakiwemo wabunge na maafisa wa ngazi za juu wa mabaraza ya mikoa na masheikh na wanavyuoni wa Afghanistan ni miongoni mwa walioshiriki kwenye maandamano hayo.
Itakumbukwa kuwa kwa mara nyingine kanisa moja lenye misimamo mikali nchini Marekani limesisitiza kuwa litachoma Qur'ani Tukufu wakati wa maadhimisho ya tarehe 11 Septemba.
Uadui na chuki za kanisa hilo la Marekani dhidi ya Uislamu ni kubwa kiasi kwamba hata limeeneza fulana aina ya "T-Shirt" na kuandika juu yake kwamba eti Uislamu ni shetani!
Juzi Jumapili pia mamia kwa maelfu ya Waislamu wa Indonesia waliandamana kulalamikia kitendo hicho cha kanisa la Marekani linaloichukia kupindukia dini tukufu ya Kiislamu. 650307
captcha