IQNA

Tukio la kuchomwa moto Qur'ani litaleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu

11:10 - September 13, 2010
Habari ID: 1992218
Jumuiya ya makundi ya kujitolea ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran imetoa taarifa kuhusu jinai ya kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani ikisisitiza kuwa tukio hilo litaleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kuwaondoa Waislamu wengi katika usingizi.
Taarifa hiyo imesema jinai hiyo inathibitisha kwamba upinzani na uhasama wa viongozi wa nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unafanyika kwa kutumia visingizio visivyokuwa na maana yoyote.
Taarifa hiyo imesema kwa mara nyingine tena chuki za nchi za Magharibi zimejitokeza katika vazi la Uzayuni na kuzijeruhi nyoyo za Waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu kote duniani. Imesema kuwa tukio la kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani limethibitisha kwamba mbegu ya mtandao wa al Qaida ambao wao wenyewe waliipanda na kudai kuwa ni nembo ya Uislamu sasa imejitokeza tena katika roho ya Magharibi kwenyewe na kuweka wazi madai ya orongo ya demokrasia na haki za binadamu.
Taarifa hiyo imesema: "Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu alisema kuhusu kadhia ya murtadi Salman Rushdi kwamba chuki na vinyongo vya Magharibi dhidi ya Uislamu inaonekana katika suala hilo kwa msingi huo Waislamu wanaweza kuhukumu vyema kwamba nara za uhuru, uliberali, haki za binadamu na kadhalika ni orongo na hadaa tupu."
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa tukio la kuchomwa moto Qur'ani huko Marekani litaleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kuwaondoa Waislamu wengi katika mghafala na kuwafahamisha kuwa uhasama wa nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unafanyika kwa visingizio visivyokuwa na maana na kwamba tatizo kubwa la Wamagharibi ni Uislamu wenyewe na Qur'ani Tukufu.
Imesisitiza kuwa kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani kinamuweka mwakilishi wa nchi za Magharibi katika eneo la Mashariki ya Kati yaani utawala wa Kizayuni wa Israel katika hali mgumu zaidi na nchi hizo zitalazimika kutumia suhula zao zaidi kwa ajili ya kulinda usalama wa utawala huo. 652942

captcha