IQNA

Serikali ya Marekani inapaswa kulaumiwa kwa jinai ya kuchomwa Qur'ani Tukufu

11:11 - September 13, 2010
Habari ID: 1992220
Mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika mkoa wa Golistan nchini Iran ametoa taarifa akilaani njama za kishetani zinazohujumu Uislamu za kundi la Wakristo wenye misimamo mikali nchini Marekani na kusema kuwa serikali ya Washington na Wazayuni ndiyo wanaopaswa kulaumiwa na kubebeshwa makosa hayo makubwa.
Taarifa ya Ayatullah Nur Mufid iliyotolewa kwa mnasaba wa njama ya kutaka kuchoma moto Qur'ani tukufu ya Kasisi Terry Jones wa Marekani imesema kuwa njama hiyo itagonga mwamba na kwamba Marekani na Wazayuni wanaojificha nyuma ya pazia ndio watakaolaumiwa kwa taathira zake mbaya na maumivu yaliyosababishwa na jinai hiyo katika nyoyo za Waislamu na wanafikra huru kote duniani.
Taarifa ya mwanazuoni huyo mkubwa wa kidini imesisitiza kuwa Qur'ani ni njia ya nuru, uongofu wa mwanadamu na mwongozo wa waumini na wacha-Mungu.
Ayatullah Nur Mufid amesema mpango uliobuniwa na kasisi jahili wa Florida nchini Marekani wa kuchoma moto Qur'ani ni dharau kubwa kwa matukufu ya Kiislamu na dini zote za Mwenyezi Mungu na unapaswa kulaani vikali.
Vilevile amezitaka jumuiya zote za Kiislamu na umma mzima wa Kiislamu kote duniani kuungana katika kukabiliana na mirengo inayuhujumu matukufu ya Kiislamu. 652953
captcha